Afisa wa polisi alijitia kitanzi katika kituo cha polisi cha Cianda kilichoko kaunti ya Kiambu mnamo Jumatatu, Agosti 30.
Kulingana na ripoti ya polisi iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Kiambu, afisa Charles Maina alijitoa uhai ndani ya nyumba yake iliyoko kituoni humo.
Tukio hilo liliripotiwa na Anthony Mwangi, afisa anayesimamia kituo hicho, ambaye alipata mwili mwenzake mwenye umri wa miaka 42 ukining'inia dirishani kulingana na ripoti ya K24.
"Aliukuta mwili wa afisa huyo ukining'inia dirishani ndani ya nyumba yake iliyoko katika kituo cha polisi cha Cianda," ripoti ya polisi ilisema.
Marehemu anasemekana alijinyonga kwa kutumia mkanda wa begi ambao alikuwa ameufunga katika dirisha hilo.
Baada ya kupata habari kuhusu kisa hicho, maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na vile vile kutoka kituo cha polisi cha Kiambu walikimbia eneo la tukio na kukuta maiti ya afisa huyo ndani ya nyumba yake.
Jamaa Adungwa Kisu Hadi Kufa Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Wenyewe
Wapelelezi walithibitisha kuwa hamna barua yoyote iliyoachwa na afisa huyo kueleza sababu za kuchukua hatua hiyo. Vile vile walisema marehemu hakuwa na majereha yoyote mwilini
Mwili wa Maina ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta kusubiri upasuaji.
Hili ni tukio la tatu la afisa wa polisi kuripotiwa kujitia uhai mwezi huu. Mnamo Agosti 10, afisa James Nderitu aliaga dunia baada ya kujiteketeza moto nyumbani kwake katika kijiji cha Mwigoyo, Kaunti ya Nyeri.
Mnamo Agosti 12, Inspekta Jenerali wa Polisi, Hillary Mutyambai, alizindua mpango wa ushauri kwa maafisa wa polisi na familia zao katika Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Wizara ya Afya pia ilielezea wasiwasi wake kwa kuongezeka kwa maradhi ya akili miongoni mwa maafisa wa usalama na kusema kuwa hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kuwasaidia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Afisi ya DP Ruto Yamwandikia Mutyambai Barua Kufuatia Kupokonywa Walinzi wa GSU
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4F1gZZmpJqrp5a5qnnYmqCbrZuWeqOtwJ2YZrGRYq6ntdKaZLCZXaW8rbXSomSkrZqewbCtjK6fmqFdoLa1wc6noGegpKK5