"Ondokeni Jubilee Sasa": Gavana Lee Kinyanjui Awaambia Murathe na Tuju

  • Kiyanjui alisema hakuna haja ya mjadala kuhusu suluhu la Jubilee akidai ni wazi tatizo ni Murathe na Tuju
  • Alisema wakati umefika kwa wawili hao kuondoka kwa hiari au watimuliwe na wenye chama
  • Gavana huyo alisema wanasiasi wa Jubilee kwa sasa wana wasiwasi kuhusu uchaguzi ujao Jubilee ikiendelea kufifia

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui amesema juhudi za kufufua ubabe wa chama cha Jubilee utaanza kwa maafisa wakuu kuondoka mamlakani.

Kinyanjui alisema kama kiongozi aliyechaguliwa anahofu kuhusu hali ya chama cha Jubilee kwa sasa.

Alisema amekuwa akishinikiza kuwe na mabadiliko katika uongozi wa Jubilee ili kipate akili mpya ya kukiendesha siku zijazo.

"Tumepeana mapendekezo hayo kwa afisi kuu na tumehakikishiwa kuwa mabadiliko yatafanywa kwa chama kuanzia mashinani hadi afisi ya juu," alisema gavana huyo.

Habari Nyingine: TBT: Picha za Rais Uhuru Kabla ya Kuomoka na Kuwa Bazuu

Kinyanjui alisema kwa sasa chama hicho kimekosa kuwika kwa sababu ya uongozi wa naibu mwenyekiti David Murathe na katibu Raphael Tuju.

Pia soma

Picha za Rais Uhuru Kabla ya Kuomoka na Kuwa Bazuu

"Tuju na Murathe siku zao ndani ya Jubilee zimeisha. Sisi ndio tumechaguliwa na sisi ndio tutashiriki katika uchaguzi ujao. Chama kikififia sisi ndio tutapoteza uchaguzi," alisema Kinyanjui.

Alisema hakuna haja ya kupoteza muda kwa sababu ni wazi kuwa tatizo kubwa la Jubilee ni uongozi.

Habari Nyingine: Mheshimiwa Gachagua Apigwa na Kibaridi Sakafubi Seli, Kushtakiwa Jumatatu

Gavana huyo alisema utafiti wake umeonyesha Jubilee bado ina wafuasi ila maafisa hao wawili wamekuwa mwiba.

"Kama kweli wanapenda chama wangekuwa wamejisajili saa hii. Kuna shida ya uongozi, ni lazima wajue kuwa Jubilee ni kubwa kuwaliko. Chama bado kina wafuasi lakini wanataka uongozi mbadala," aliongeza.

Wawili hao walijipata pabaya baada ya Jubilee kupoteza viti katika chaguzi ndogo kadhaa zilizofanyika mwezi Mei na Julai.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoZ6gJBmpqecn6Cyr7WMo6yboZyasm6%2FwKyYZp%2BRq66vrYylnJ5lm567uq3No6yiZZGsrqK5waKYZqWlp661tMRmpZplpKq3tnrHraSl