Man United Waweka Historia Kukamilisha Kampeni Bila Kichapo Ugenini

- Licha ya kupoteza ufalme wa Ligi Kuu kwa mahasidi wao Man City, Ole atajivunia masogora wake kukamilisha kampeni bila kupokezwa kichapo ugenini

- Kocha huyo mzawa wa Norway aliteua kikosi imara wakati wa mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Wolves huku akiwapendelea makinda

- Makinda hao walitimiza imani na matokeo ya kuridhisha wakisajili ushindi wa 2-1 ugani Molineux

- Ushindi wa United uliwashuhudia wakiweka historia wakijiunga na Arsenal kwenye orodha ya vilabu kumaliza kampeni bila kupokezwa kichapo ugenini katika mechi ya EPL

- Gunners waliweka rekodi hiyo msimu wa 2002/03 kabla ya kushiriki kampeni mpya bila kichapo nyumbani na ugenini

Habari Nyingine: Christiano Ronaldo Apiga Hatua Kubwa Kurejea EPL Kusakatia Man United Soka

Man United wamefunga jamvi ya kampeni ya msimu wa 2020/21 ya Ligi Kuu Uingereza kwa njia ya kipekee wakipiga Wolves 2-1 ugani Molineux Jumapili, Mei 23.

Licha ya kukamilisha kampeni kwenye nafasi ya pili, kulikuwa na kila sababu ya United kujivunia kuswaga vijana wa Nuno Espirito ugenini.

Endapo wangelipata ushindi ama ushinde, Mashetani Wekundu wamekamilisha kampeni bila kuchapwa ugenini ambapo ni historia ya kwanza kwa klabu hiyo.

Habari Nyingine: Mbwembwe Mtoto Mkenya Leo Messo Akijiunga na Klabu ya Arsenal

Huku wakiwa wameratibiwa kuvaana na Villarreal kwenye UEFA siku chache zijazo, Ole Gunnar Solskjaer aliamua kuwapumzisha baadhi ya masogora wake wakuu na kuwatumia makinda kung'aa.

Anthony Elanga akifungua ukurasa wa mabao kwenye mechi yake ya kwanza na timu ya watu wazima ya United.

Hata hivyo, Nelson Semedo alisawazishia Wolves kabla ya Juan Mata kuwafungia waajiri wake bao la ushindi dakika za lala salama.

Vijana wa Solskjaer walifaulu kutetea ushindi wao ambao uliwasaidia kuhifadhi nafasi ya pili jedwalini na kujiunga na Arsenal kwenye rekodi ya kukamilisha msimu bila kupokezwa kichapo ugenini.

Gunners waliweka rekodi hiyo msimu wa 2002/03 kabla ya kushiriki kampeni mpya bila kichapo nyumbani na ugenini.

Akitoa maoni kuhusu mechi hiyo, Solskjaer alikiri kuwa anajivunia ushindi huo wa kukamilisha kampeni.

Ushindi huo uliwashuhudia United wakikamilisha kampeni na tofauti ya alama 12 nyuma ya mahasidi Man City ambao walitawazwa wafalme wa msimu huu.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoBxgZNmpJqmXaq7qsDEnWSwmaeauKJ5x6Kqraeinq5ut9SkmKahnJ7Aqa2MpJimqJWjtm6uyKWYZqOZmLWivM5mrKCdnp67qnrHraSl