- Mwanafunzi huyo pamoja na mwenzake walinaswa baada ya kufumaniwa wakijaribu kuteketeza bweni la shule hiyo
- Wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Manyatta wakiendelea kuhojiwa kuhusu kisa hicho na maafisa wa polisi
- Kamanda wa Polisi wa Embu Daniel Rukunga alisema risasi hiyo ni ya bunduki aina ya AK-47
Habari Nyingine: Orodha ya wawaniaji 13 wanaopigania kiti cha Jaji Mkuu David Maraga
Polisi katika kaunti ya Embu wanamzuilia mwanafunzi mmoja ambaye alipatwa na risasi katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Kamama.
Mwanafunzi huyo pamoja na mwenzake walinaswa baada ya kufumaniwa wakijaribu kuteketeza bweni la shule hiyo.
Walikamatwa na sasa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Manyatta wakiendelea kuhojiwa kuhusu kisa hicho na maafisa wa polisi.
Habari Nyingine: Jamaa aliyejifanya polisi na kujaribu kumnasua mwenzake katika seli anaswa
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa Leo, Alhamisi, Februari 11, wanafunzi hao watafikishwa kortini kujibu mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika.
Kulingana na simulizi ya mmoja wa walimu wa shule hiyo, mlinzi wa shule aliyekuwa kwenye zamu aliwaona wawili hao karibu na bweni la shule usiku na kujaribu kuwafuata lakini walichana mbuga.
Wakati huo huo, mlinzi huyo aliona wingu la moshi likitokea kwenye bweni moja na alipokaribia, moto ulikuwa umewashwa chini ya kitanda lakini ulizimwa.
Alipiga ripoti kwa Mwalimu Mkuu ambaye aliwaita wanafunzi hao na katika harakati ya kuwakagua alimpata mmoja wao na risasi mfukoni.
Kisha aliwaita maafisa wa polisi ambao waliwakamata wawili hao na kuwapeleka stesheni.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Embu Daniel Rukunga alisema risasi hiyo ni ya bunduki aina ya AK-47.
Uchunguzi umeanzishwa kutambua namna mwanafunzi huyo alipata risasi hiyo na mmiliki wa bunduki hiyo.
Haya yanajiri siku chache baada ya Chama cha Kitaifa cha Walimu Kenya (KNUT), kimepinga vikali pendekezo la Waziri wa Elimu George Magoha la kurejesha adhabu ya viboko shuleni.
Akizungumza mjini Nakuru, Katibu Mkuu wa KNUT Wilson Sossion alisema kurejesha adhabu ya viboko shuleni kutazua mkwaruzano kati ya wanafunzi, walimu na wazazi.
Sossion alipendekeza kuwa endapo serikali inataka kurejesha viboko, lazima maafisa wa polisi watumwe shuleni kutekeleza adhabu hiyo akihofia kuwa wanafunzi wanaweza kugeuka na kuua walimu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZX93fJRmpLCZnpaztrrZomSaqJGptqytzZpkp5ldp7a0rdKiZKygpaGyr7WMnqSbrV6dwa64