Rais Uhuru awasili kwenye Ikulu ndogo ya Sagana

- Rais atakuwa Sagana kwa siku nne kuanzia Ijumaa Januari 29 hadi Februari 1 ambapo BBI itachambuliwa

- Viongozi wanaomuunga mkono ndio walialikwa kwenye kikao hicho huku Tangatanga wakiachwa nje

- Mkutano huo wa Sagana umewasha joto la kisiasa na matokeo yake yanatarajiwa pakubwa

Rais Uhuru Kenyatta amewasili kwenye Ikulu ndogo ya Sagana ambapo mkutano wake na viongozi wa Mlima Kenya unatarajiwa kuanza hii leo.

Kulingana na wandani wa Rais, Uhuru atakuwa na MCAs ambapo watachambuliwa mswada wa BBI huku akiwarai kuunga mkono utakapopelekwa kwenye kaunti.

Baadaye Rais Kenyatta atakutana na wabunge wote kutoka eneo la Mt Kenya ili kupigia debe ripoti hiyo na kuwataka waunge mkono mchakato wa mabadiliko ya kikatiba.

Jumamosi Rais atakutana na viongzoi wengine wa mashinani na kisha vijana katika kampeni zake za kuendelea kuwarai wamfuate kisiasa.

Habari Nyingine: Gavana Hassan Joho atangaza atawania urais 2022: "Nimempigia Raila debe kwa muda mrefu"

Mkutano huo wa Sagana umewasha joto la kisiasa ndani ya ngome ya Rais baada ya wandani wa Naibu Rais William Ruto kutoalikwa.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria alisema kikao hicho ni cha kuendeleza ajenda potovu za kambi ya Kieleweke.

"Mkutano huo mnasikia wa Mt Kenya Sagana ni wa kambi ya Kieleweke. Wabunge wa Tangatanga hawajaalikwa. Ni njama tu nyingine ya watu ambao wamemteka Rais Uhuru Kenyatta," Kuria alisema.

Habari Nyingine: Raila afanyiwa 'madharau' Githurai na habari zingine zilizozua gumzo wiki hii

Wabunge 41 ambao hawakualikwa kwenye mkutano huo walimwandikia Rais Uhuru barua na kumkashifu vikali kwa siasa zake za hivi maajuzi.

Walisema amekuwa akitaka kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga na kumpigia debe kwa watu wa Mt Kenya.

Kwenye barua hiyo, walimkumbusha Rais pia kuwa aliwafunza kumlima kisiasa Raila na kwa hivyo hawawezi kuanza kumuunga mkono.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZX50fpVmqZqho2LCqcHRrmSar5Gotq21jKSunqapmnqqt9SlrGamlKS0sHnYmmSsmZeWu6J6x62kpQ%3D%3D