Moses Kuria apatwa na coronavirus

- Moses Kuria amekuwa katika hospitali ya Karen kwa siku 27 akipambana na maradhi ya Covid-19

- Alisema yale amepitia yamembadilisha na sasa anataka Wakenya kuangazia kupambana na janga hilo badala ya sarakasi zinazoendelea

- Kuria alisema wahudumu wote wa afya wanapitia katika hatari kubwa katika kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa maradhi ya coronavirus.

Kuria alifichua amekuwa akipokea matibabu kwa siku 27 zilizopita katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.

Habari Nyingine: Orodha ya watu 9 ambao Matiang'i amesema wanafadhaili ugaidi

Alisema hayo Jumatano Septemba 2 kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuchapisha picha akipokea matibabu.

Alisema ni wakati Wakenya kuamini kuwa ugonjwa huo upo na kuendelea kujikinga ipasavyo.

"Natumai kuwa licha ya mjadala unaoendelea kuhusu Covid-19, hakuna atakayesahau kuwa ugonjwa wa coronavirus upo. Makosa makubwa tunayoweza kufanya ni kuacha kujilinda," alisema.

Habari Nyingine: Mbunge Bobi Wine ashtakiwa kwa kudanganya kuhusu umri wake

Kuria alitoa heko kwa maafisa wote wa afya ambao wanashughulikia wagonjwa wa Covid-19 akisema wanaweka maisha yao katika hatari kubwa.

"Wacheni tuwakumbuke wanajeshi wetu wote ambao wanaongoza vita dhidi ya coronavirus kwani wanaweka maisha yao hatarani kuwahudumia wagonjwa wa coronavirus," alisema Kuria.

Aidha mbunge huyo alisema kupatwa na maradhi hayo kumebadilisha msimamo wake kwenye suala hilo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIR3f5BmpKirlah6rMHRophmmaCWwbitjKeYZpufp7yvrdWiqa6rXp3Brrg%3D