Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) lilionekana kufurahi sana baada ya rubani wake wa kike kushinda tuzo la Bara la Afrika.
Rubani Irene Koki Mutungi ni miongoni mwa marubani wa kike ambao wanaaminika kuwa mfano mzuri kwa wasichana wa umri mdogo nchini.
Katika ukurasa wake wa Facebook Jumanne, Juni 19, KQ ilishindwa kujizuia baada ya Koki kushinda tuzo la Top Travel 100 Women Barani Afrika.
Habari Nyingine: Wakili anaswa akitazama video 'chafu' mahakamani
"Leo, mmoja wetu Cpt. Irene Koki Mutungi anapokea tuzo kutoka kwa Wizara ya Utalii kama mshindi wa Africa Top Travel 100 Women," ilisema KQ katika tangazo hilo.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Binti huyo pia ndiye rubani wa kwanza wa kike Barani Afrika kuendesha Boeing 787. Tuzo hilo alilipokea kutoka kwa Afisa Mkuu wa Operesheni wa KQ Jan De Vegt na mkurugenzi wa shughuli za ndege Captain Njoroge.
Habari Nyingine: Mwanamume afumaniwa akijifanya mwanamke kuwanyemelea wanaume wenzake (picha)
Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walimshangilia rubani huyo kwa kumtumia jumbe la kumpongeza.
Wengi walisema alistahili tuzo hilo, na hata kumwita ‘Pride of Africa’. Koki na rubani mwenzake Sally Ombewa hupeperusha Boeing 787 kati ya Nairobi, Kenya na London, England.
Habari Nyingine: Bintiye Najib Balala anavutia sana, na kulandana kabisa na babake
Mabinti hao wawili wameshangiliwa na Wakenya na kuelezewa kama mfano mwema kwa mtoto msichana.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIR0fJdmqa6akaO2bsPAZqKio5VixKJ5yp6lspldlrazw8Cyqmajn6C2brnUraynn5lirrS0yKebmmWkqsewecyun6KlpWKup77IpJhnoKSiuQ%3D%3D