Mchanganuzi wa NMG ajiondoa kwa misingi ya serikali kuvihangaisha vyombo vya habari

- Mchanganuzi na mwanahabari katika NMG amewakashifu wakuu wa shirika hilo la habari kwa kushirikiana na serikali badala ya kufanya kaz zao inavyostahili

- Kundoka kwa Maina Kiai kunajiri mwezi mmoja tu baada ya David Ndii kuonyeshwa mlango na NMG kama machanganuzi mkuu

Nation Media Group (NMG) imepata pigo kubwa baada ya wachanganuzi na waandishi wakuu wenye usemi nchini kuondoka ghafla.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Nane hao katika taarifa ya kijumla iliyoonekana na TUKO.co.ke siku ya Jumanne, Machi 27, wachanganuzi hao walisema kuwa wameondoa huduma zao katika shirika hilo haswa Daily Nation wakisema kuwa serikali inaingilia sana utendakazi wa shirika hilo na vyombo vya habari kwa jumla.

Habari Nyingine: Raila anaswa kwenye video akivurugana na polisi JKIA baada ya Miguna kuzuiliwa

Mkurugenzi wa tume ya kutetea haki za kibinadamu, Maina Kiai ndiye wa hivi punde kujiondoa kama mwandishi na mchanganuzi wa masuala nbalimbali siku ya Jumanne, Machi 27, 2018.

Kulingana na barua ya kujiuzulu aliyoandika yenye mada kuwa 'Tumekataa kunyamazishwa', mabosi wa NMG wameungana na serikali na kusahau majukumu yao ya kuwajibikia uhuru wa vyombo vya habari.

Habari Nyingine: Video ya kusisimua ya aliyekuwa mchumba wa Diamond akiogelea yawaacha ‘mafisi’ taabani

Barua hiyo iliyokuwa imetiwa saini na wote wanane; Maina Kiai, Muthini Wanyeki, Gabriel Dolan, Rasna Warah, Goerge Kegoro, Kwamchetsi Makokha, Gabrielle Lynch na Nick Cheeseman, ililalama kuwa wakuu wa NMG walikuwa wakizitupilia mbali taarifa za wanahabari na wachanganuzi zinazoigonga serikali.

Habari Nyingine: John Allan Namu akiri kudanganya katika uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenziwe

Kuondoka kwao kunajiri mwezi mmoja baada ya mabosi hao kumfuta David Ndii kutokana na joto kali la kisiasa iliyokuwa imetawal nchini.

Mwezi huo huo ambao Ndii alifutwa kazi, Linus Kaikai aliyekuwa mkurugenzi wa NTV alijiuzulu.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa moto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4Z4fpZmpJygkaO0orrUs6Bmr5Fiu66zjJqhoqeembyiecqwmGalmai2r7PIZrCaZaOav6q3wKWgZqOlq7aprc2gmKKrmJZ6t8XOppmoZaaurm60wJuYq6FencGuuA%3D%3D