Mbunge awafurahisha wenyeji kwa kuwaoshea watu magari

-Mwanasiasa anayehudumu kwa mara ya kwanza kama mbunge wa Kisumu ya Kati Fred Ouda amewafurahisha wenyeji kwa kuwaoshea watu magari

-Mbunge huyo alijitokeza na kuwasaidia wanaoosha magari katika kituo kimoja eneo hilo kufanya kazi hiyo

-Huku wengine wakimsifia, wengine walimkashifu kwa kutafuta umaarufu katika sehemu isiyostahili

Mbunge wa Kisumu ya Kati Fred Ouda aliyegonga vichwa vya habari kwa kuvua mavazi yake mbele ya wanahabari baada ya kukerwa na matusi yalioelekezewa Raila Odinga amewazingua Wakenywa tena.

Mbunge huyo ameangaziwa tena akiripotiwa kuwasaidia wenyeji wa Kisumu kuyaosha magari yao katika kituo kimoja cha kuosha magari eneo hilo.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Babu Owino azungumzia "ulevi" wa Mbunge Moses Kuria

Habari Nyingine: Serikali yatoa taarifa kuhusu afya ya rais mstaafu Daniel Moi

Baadhi ya Wakenya hawakufurahishwa na mbunge huyo wakidai kuwa alikua akitafuta umaarufu katika sehemu zisizostahili.

“Fred Ouda, hii sio kazi ya mbunge. Hutapata umaarufu kisiasa kwa kufika kwenye kituo cha kuosha magari na kuwaoshea watu magari. Kazi yako ni uwakilishaji.” Aliandika Eric Ochanji kwenye kipachiko alichokwisha kukifuta.

Habari Nyingine: Huyu ndiye 'Mr Nakuru'; barobaro anayewazingua wanawake kwa tabasamu lake

Baadhi ya Wakenya walifurahishwa na hatua ya mbunge huyo ya kutangamana na watu wakiitaja kama njia ya kipekee ya mbunge huyo kujua matatizo ya watu wa eneo bunge lake.

Mbunge huyo alionekana akiwa amevalia kaptura na vesti akiyaosha magari ya wateja kama wahudumu wa wengine wa kuosha magari na wakati mwingine kupiga gumzo nao chini ya mti.

Habari Nyingine: Vitu 5 vinavyoweza kumfanyikia William Ruto kutokana na mkutano wa Uhuru na Odinga

Hii si mara ya kwanza kwa Ouda kugonga vichwa vya habari, kwani aliwahi kumzaba kofi kamanda wa polisi wa kaunti ya Nairobi nje ya mahakama ya juu zaidi nchini baada ya uchaguzi wa Agosti 8, 2017, akimkumbusha kuwa maandamano ya amani yameruhusiwa na katiba.

Ouda alikuwa mtu wa tatu kumzaba kofi afisa wa ngazi ya juu wa polisi baada ya Bernard Chunga na Babu Owino.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa moto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4V5hZJmpJutnpyybq3Wmp2uqpGdtrS0wGaunqapmreqecqwmGajpayusL%2FHnphmr5Gpwm65wKCYq6FencGuuA%3D%3D